MALI ZILIZOPATIKANA KWA NJIA YA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU ZATAIFISHWA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam imeamuru mali za Pastory Francis Mayila, mhasibu wa Kampuni ya UEE Tanzania, zitaifishwe, baada ya kupatikana na hatia ya makosa 4 ya kughushi na moja la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu bila kuwepo mahakamani.

Amri hii imetolewa hivi karibuni (tarehe 27/2/2017) na mahakama chini ya Hakimu Mkuu Mkazi mheshimiwa Respicius Mwijage kufuatia  ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Pastory Francis Mayila ambaye alitoroka uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU na mashtaka aliyofunguliwa na Jamhuri.Tarehe 16Machi,2016 Mayila alifunguliwa na Jamhuri mashtaka ya  Makosa 4 ya kughushi na moja la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu bila kuwepo mahakamani. Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwakiliswa na Mwanasheria Shadrack Martin Kimaro alikisaidiwa na Mwanasheria Max Ari toka TAKUKURU.

Mali zilizoamriwa na mahakama zitaifishwe na Serikali ni magari 4(Toyota Chaser T349 AQJ,Toyota Chaser T264 AWA, Toyota Landcruser T896 ASC, na Mitsubish Fuso T265 AWM); nyumba (5 zilizoko Buhongwa, Nyamagana, Mwanza, na 1 iliyoko Ilemela, Mwanza) na eka 5 za ardhi zilizoko Mwandu, Nyamagana, Mwanza.

Kati ya tarehe 29Agosti, 2008, 30 Oktoba, 208, 27Novemba, 2008 na 29Desemba, 2008 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kufanya udanganyifu mshtakiwa alishiriki kughushi malipo na form za  kuhamisha fedha-TISS (Tanzania Interbank Settlement System). TTCL ilikusudia kuhamisha fedha toka kwenye akaunti yake iliyoko benki ya NBC kwenda kwenye akaunti ya TRA iliyoko BOT na badala yake mshtakiwa na washirika wake walizielekeza fedha hizi kwenye akaunti ya kampuni ya UEE iliyoko benki ya Standard Chartered katika viwango tofauti vya fedha vyenye jumla ya Tsh.3,392,812,190.28/= baada ya kughushi form za TISS. Kiasi hiki cha pesa kilikusudiwa  na TTCL kulipa kodi ya ongezeko la Thamani kutokana na huduma zilizotolewa na kampuni kwa miezi ya Agosti, Oktoba, Novemba,  na Desemba, 2008. Mshtakiwa alishirikiana na watu wengine 5katika kutenda uhalifu huu ambao tarehe 17Januari, 2017 walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 5 jela au kulipa faini ya Tsh.100,000,000/= katika shauri la jinai namba 157/2010. Mshtakiwa alishtakiwa peke yake kwa vile alitoroka uchunguzi.

Aidha, kati ya mwezi Agosti, 2008 na Februari, 2009 ndani ya jiji la Dar es Salaam mshtakiwa akiwa na  nia ovu ya kufanya udandanyifu  alijipatia jumla ya Tsh.362,700,000/= toka TRA kwa maelezo kwamba alistahili kulipwa wakati si kweli.

Maombi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali  kutaifisha mali za mshtakiwa yalifanywa chini ya kifungu 9(1)(a)  cha Sheria ya Mapato yatokanayo na Uharifu(Proceeds of Crime Act, CAP 256 R.E. 2002).

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail