Dkt Hoseah na rushwa katika uchaguzi

dr hoseah 2

MKURUGENZI MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, amejitapa kuwa mgombea yeyote atakaye toa rushwa kwa wapiga kura ili apigiwe kura atawashughulia. Anaandika Jimmy Mfuru… (endelea).

Kauli hiyo ya Dkt Hoseah inakuja wakati kura za maoni kuwapata wagombea wa nafasi za ubunge unaofanywa na baadhi ya vyama mbalimbali huku Chama Cha Mapinduzi CCM kikionyesha kuongoza kwa kutoa rushwa katika mchakato huo.

Dk.Hoseah amesema kipindi hiki haponi mtu kwa atakayetoa au kupokea rushwa na kwamba atawashughulikia bila kujali nafasi zao na kuwaonya wananchi wasidanganywe kwa kuuza utu wao kwa kuhongwa na wagombea kwa kuwa kufanya hivyo ni kununuliwa utu wao.

“Kipindi hiki Takukuru hatuna mchezo kwa yeyote atakayetoa wala kupokea rushwa kipindi hiki hakuna biashara ya wananchi kuwaambia wagombea sasa unaniacheje ni marufuku tutawashughulia”amesema Dk.Hoseah.

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail