AFISA WA TRA NA YONO AUCTION MART WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA

matapeli

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 25/4/2016 imewafikisha Mahakamani Bw. Amani Samson Mkwizu, afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bw. Edward Nyakamwe Magobela, mtumishi wa Yono auction Mart kwa makosa ya Rushwa na Utapeli kinyume na kifungu Na. 15(1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana Na Rushwa na 11 ya mwaka 2007.

Washitakiwa hao pamoja na watuhumiwa wengine wawili (2) ambao hawakuwepo mahakamani leo wanaiwa kwamba mnamo tarehe 19/4/2016 jijini Dar es Salaam, walimshawishi Bw. Glenn Clarke, Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Commercial Sales and Services Tanzania Limited’ kutoa rushwa ya TShs. Milioni Hamsini (50,000,000/-) ili waweze kumsaidia kuongea na wakubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupunguza deni la Kodi la Kampuni yake kutoka Milioni Mia Tatu Sabini na Tano (375,000,000/-) kufikia Milioni Mia Moja (100,000,000/-). Katika kosa linguine washtakiwa hao walipokea Tshs Milioni tatu (3,000,000/-) kama sehemu ya Tshs. 100,000,000 walizoomba kutoka kwa Bw. Clarke.

Wakili wa TAKUKURU Dennis Lekayo aliwasomea mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Huruma Shahidi ambapo walifunguliwa kesi ya Jinai Na. 145/2016.

Mshtakiwa wa kwanza Bw. Mkwizu yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana na Bw. Magobela ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo yupo rumande. Kesi hii itatajwa tena tarehe 9/5/2016

IMETOLEWA NA

OFISI YA AFISA UHUSIANO, TAKUKURU MAKAO MAKUU

25 April, 2016

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail