Courtesy call from Danish Ambassador to PCCB

 

NDC Study tour at PCCB

https://mail.pccb.go.tz/?_task=mail&_action=get&_mbox=INBOX&_uid=540&_part=2&_mimewarning=1&_embed=1&_extwin=1

 

Ag. Director General, Valentino Mlowola -CP, NDC  Commandant,Brig. Gen. J.M Mwasela in a picture with PCCB Directors and NDC delegation
when visited PCCB HQ January 29th, 2016

TGCL students visit PCCB

https://mail.pccb.go.tz/?_task=mail&_action=get&_mbox=INBOX&_uid=539&_part=2&_mimewarning=1&_embed=1&_extwin=1

 


Ag. Director General,Valentino Mlowola -CP in a picture with the University of Dar es Salaam Students under the Tanzanian- German Centre for eastern African Legal Studies (TGCL), when they visited PCCB Head quarters on 27th January, 2016. Students are from Tanzania,Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan.

TAKUKURU yawaonya watumishi, wananchi, wafanyabiashara wanaojihusisha na rushwa

  • Kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa rushwa kubwa

https://mail.pccb.go.tz/?_task=mail&_action=get&_mbox=INBOX&_uid=533&_part=3&_mimewarning=1&_embed=1&_extwin=1

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika Januari 26, 2016 katika ukumbi wa TAKUKURU Makao Makuu.

 

 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewatahadharisha watumishi wa umma, wananchi na wafanyabiashara kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa kuwa chombo hicho hakitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na taratibu.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Januari 26, 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola aliwataka watumishi wa umma wanaojihusisha na rushwa kwa maslahi binafsi watafakari kabla hawajafanya hivyo. Aliwashauri watumishi hao kuwa iwapo hawawezi kufuata taratibu za utumishi wa umma wajiondoe na kuwaachia nafasi hizo watanzania wengine ambao hawana kazi ili wawatumikie wananchi kwa uadilifu.

Wananchi sasa hivi wana kiu ya kupata maendeleo na maisha bora, watumishi wa umma watambue kwamba wanannchi wa jana siyo hawa wa leo kwani wamedhamiria kuunga mkono jitihada hizi za Serikali yao ya Awamu ya Tano za kuwaletea maendeleo na maisha mazuri. Hivyo yeyote yule atakayethubutu kuhujumu jitihada hizi za Serikali na kujihusisha na vitendo vya rushwa ataripotiwa tu, nasi hatutosita kuchukua hatua stahiki,” alifafanua Kamishna Mlowola.

Alifafanua kuwa watumishi hao wa umma ni pamoja na watumishi watoa huduma katika ofisi yoyote ya umma, maofisa maduhuli, wakusanyaji wa kodi, maofisa manunuzi na watumishi wengine wanaohusika na kutumia fedha za umma ambao wote aliwataka kufanya kazi kwa weledi na uaminifu. Alisema TAKUKURU itawachunguza na kuwafungulia mashtaka watumishi wote watakaotumia vibaya fedha na rasilimali za umma ikiwa ni pamoja na kuwafilisi mali ili kurejesha hasara waliyoisababishia Serikali. “…tutachukua hatua mara moja na nawaomba wananchi watuunge mkono kwa kutupatia taarifa mara moja,” alisisitiza Kamishna Mlowola.

Akielezea mafanikio yaliyopatikana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU alifafanua kuwa muitikio mkubwa wa wananchi kutoa taarifa za rushwa, ni matokeo ya jitihada za kuelimisha umma kuhusu rushwa na madhara yake kwa jamii. Hata hivyo, alisema jambo hili limewezekana kwa vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele kusambaza habari na elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Alisema waandishi wa habari ni wadau muhimu na kuahidi kushirikiana nao ili kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.

https://mail.pccb.go.tz/?_task=mail&_action=get&_mbox=INBOX&_uid=533&_part=4&_mimewarning=1&_embed=1&_extwin=1

Waandishi wa habari wakichukua kumbukumbu katika mkutano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola uliofanyika Januari 26, 2016 katika ukumbi wa TAKUKURU Makao Makuu

Kamishna Mlowola alisema TAKUKURU inakamilisha uchunguzi wa rushwa kubwa 36 ambapo nyingine kati ya hizo zimekamilika na kuombewa kibali cha kuwafikisha mahakamani kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Akifafanua kuhusu baadhi ya kashfa ya rushwa zilizoripotiwa na kuzungumziwa na wananchi, Kamishna Mlowola alisema kuwa mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ametakiwa kulipa kodi ya shilingi bilioni 8.5 katika kipindi cha miezi miwili na akishindwa atafikishwa mahakamani. Lake Oil ilifanya udanganyifu na kukwepa kodi hiyo baada ya kuuza mafuta ya petroli lita 17,461,111.58 katika soko la ndani ya nchi ambazo ilidanganya kuwa zimesafirishwa kwenda katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Alieleza pia kuwa TAKUKURU inakamilisha kashfa ya rushwa inayohusu malipo ya fedha dola za kimarekani milioni sita kwa kampuni ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA) kwa madai ya kuisaidia Tanzania kupata mkopo wa fedha za kimarekani milioni 600. Kamishna Mlowola alifafanua kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa fedha hizo, dola za kimarekani milioni sita, zilitakatishwa kwa ushirikiano wa watumishi wa umma na wa sekta binafsi huku wakifahamu kuwa fedha hizo wamezipata kwa njia haramu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU alieleza kuwa Taasisi inaendelea na imekamilisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za rushwa kuhusu Shirika la Reli Tanzania (TRL). Hizi ni pamoja na ile ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za kuwapata wazabuni katika ujenzi wa reli ya kisasa ya kimataifa (standard gauge) uliosimamiwa na Shirika Hodhi la Reli nchini (RAHCO) na ile ya ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 21/2004 wakati wa ununuzi wa mabehewa 25. Alisema TRL iliagiza mabehewa hayo kutoka India ambayo hayakuwa katika viwango vilivyokubalika katika mkataba na bado ikiwalipa bilioni za shilingi. Wahusika katika mchakato wa ununuzi huo watafikishwa mahakamani.

Kamishna Mlowola aliwaambia waandishi wa habari kuwa TAKUKURU imejipanga kutekeleza majukumu hayo ya kisheria na azma na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kupambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo bila ya kumuonea wala kumuogopa mtu yeyote.

https://mail.pccb.go.tz/?_task=mail&_action=get&_mbox=INBOX&_uid=533&_part=5&_mimewarning=1&_embed=1&_extwin=1

Bw. David Ramadhani, mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten akiuliza swali wakati wa mkutano wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola na waandishi wa habari uliofanyika Januari 26, 2016.

Naomba nisisitize hapa kwamba Mheshimiwa Rais alipozungumza kwamba amejipa kazi ya ‘kutumbua majipu’ tambueni kwamba TAKUKURU ndiyo vidole vya Mheshimiwa Rais katika kuyatumbua ‘majipu hayo.’ Kasi ya kufanya shughuli hiyo ni yetu TAKUKURU na nataka muelewe kwamba mwenye vidole akishaamua kutumbua ‘jipu’ kazi ya vidole ni utekelezaji tu. Na niwahakikishie kwamba tuko tayari kwa hilo,” alisisitiza Kamishna Mlowola.

Waziri Kairuki aitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa bidii, kufuatilia rushwa ndogo na kuwa mfano kwa uadilifu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angela Kairuki amewataka watumishi wa TAKUKURU kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia misingi ya kazi na taaluma ya uchunguzi ili kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Mhe. Kairuki aliyasema hayo Januari 4, 2016 wakati akiongea na watumishi hao katika ukumbi wa TAKUKURU Makao Makuu, jijini Dar es Salaam. Alifafanua kuwa haina budi kwa Taasisi kupima utendaji wake wa kazi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975 kikiwa Kikosi cha Kuzuia Rushwa hadi sasa na kujipanga kutekeleza majukumu yake kwa namna itakayoleta tija zaidi.

Waziri Kairuki aliipongeza Taasisi kwa utendaji mzuri na kueleza kuwa pamoja na kuwa na kesi nyingi za rushwa kubwa, TAKUKURU ifanye chunguzi zake vizuri na itoe kipaumbele pia kwa rushwa ndogo. “Nadhani mnakumbuka tukio la Igunga, Tabora? Hivi yule daktari alishindwa nini kumuhudumia yule mtoto pasipo kwanza kudai rushwa? Hizi pamoja na kuitwa rushwa ndogo, ni kero kubwa kwa wananchi wengi…,” alisisitiza Waziri.

Hata hivyo alitahadharisha kuwa utekelezaji huo wa majukumu uzingatie haki, misingi ya kazi na taaluma ya uchunguzi. “Usikamate mtu kwa hila… Ni bora kuwaachia wahalifu mia moja kuliko kumsingizia mtu mmoja asiye na hatia na kufungwa,” alisema Mhe. Kairuki. Pia alishauri TAKUKURU ishirikiane vizuri na vyombo vingine vya kutoa haki ili kuinua utendaji kazi.

Waziri huyo wa Utumishi na Utawala Bora aliwaeleza watumishi hao kuwa ingawa TAKUKURU ni chombo cha uchunguzi, lakini watumishi wake wanalalamikiwa na kutuhumiwa kwa rushwa. Aliitaka Taasisi hii iwe mfano mzuri katika utawala bora na kwamba wale watumishi wanaojua kuwa si waadilifu wajirekebishe au wajiondoe wenyewe. Mhe. Kairuki alisema kuwa ili kudumisha uadilifu atatumia vyombo vingine vya uchunguzi kuwachunguza watumishi wa TAKUKURU.

Waziri Kairuki aliagiza kuwa hotuba ya Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kufungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isomwe tena kwa makini na itumike katika kujipanga kutekeleza majukumu ya TAKUKURU. Alichukua fursa hiyo kuwataka watumishi wote kufuatilia mijadala ya Bunge.

Alisema yeye yupo pamoja na Taasisi hii na kuwa Rais, Mhe. Dkt. Magufuli anaitegemea TAKUKURU katika kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa nchini. Hivyo, aliwataka watumishi wote kuchukua hatua za kiutendaji mapema kabla ya matukio na kuwa wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao. Aidha, aliahidi kushughulikia kero za watumishi zinazohusiana na ajira, vyeo na maslahi ya kazi hata hivyo akawakumbusha kuwa pamoja na kuwa na haki na stahili za kikazi, watumishi wana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi.

Awali, akitoa maelezo ya utangulizi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola alieleza kuwa katika kutekeleza majukumu yake ya kuzuia na kupambana na rushwa mwaka 2015, Taasisi iliikoa zaidi ya shilingi bilioni saba kupitia chunguzi mbalimbali zilizofanyika. Fedha hizi ilikuwa zitumike kwa njia ya rushwa kinyume na ilivyopangwa.

Pia alieleza kuwa TAKUKURU iliendelea na kuelimisha umma kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wake katika mapambano dhidi ya rushwa na kufanya tafiti ili kubaini mianya ya rushwa. Kamishna Mlowola alifafanua kuwa mapendekezo hutolewa kupitia tafiti hizo ya jinsi ya kuziba mianya ya rushwa ingawa siyo taasisi zote hutekeleza mapendekezo jambo ambalo ni changamoto katika kufanikisha azma ya kuimarisha mifumo ya kutoa huduma bora kwa umma.

Kikao hicho kati ya Waziri Kairuki na watumishi wa TAKUKURU kilihudhuriwa na watendaji wa ngazi zote za TAKUKURU Makao Makuu na mikoa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wakiwemo Wakurugenzi wa Idara, Wakuu wa Vitengo, Wakuu wa Sehemu na Wakuu wa TAKUKURU Mikoa.