- USHIRIKI WA VIJANA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.
TAKUKURU imekuwa ikishirikisha vijana katika mapambano dhidi ya rushwa kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kwa njia ya semina, matamasha ya sanaa, midahalo, Mikutano ya Hadhara, Uchoraji Katuni, Utunzi wa Insha au Mashairi na Mijadala ya wazi. Pia vijana wamekuwa wakishiriki kwenye vipindi vya redio na televisheni.
- UANZISHWAJI WA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA.
Mnamo mwezi Mei, 2007 TAKUKURU ilianzisha kampeni ya kufungua klabu za wapinga rushwa katika shule za sekondari Tanzania Bara ambapo Mkurugenzi Mkuu alizindua klabu ya wapinga rushwa shule ya Sekondari Makongo kama ishara ya kuanza rasmi kampeni hii.
Hata hivyo, ujenzi wa maadili unatakiwa kuanzia ngazi ya msingi, hivyo Mnamo mwezi Julai , 2013 TAKUKURU iliona ni vema klabu hizi zikaanzishwa katika shule za msingi. Hii itasaidia kuleta mabadiliko ya kijamii hususani katika kubadili mtazamo wa jamii kutoka kwenye mtazamo kuwa rushwa ni sehemu ya utamaduni na kuiona rushwa kuwa ni tatizo la kitaifa lisilotakiwa kuvumiliwa kwa namna yoyote. Ili rasilimali hii iweze kutumika vizuri zaidi, kuna umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza klabu katika shule za msingi.
- TAKWIMU ZA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA.
IDADI YA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA ZILIZOFUNGULIWA TANGU MEI 2007 HADI JUNI 2016
MWAKA | S/MSINGI | SEKONDARI | VYUO | JUMLA | ||||
Idadi | Wanachama | Idadi | Wanachama | Idadi | Wanachama | Idadi | Wanachama | |
2007 | 1284 | 65,518 | 1284 | 65,518 | ||||
2008 | 347 | 22,439 | 347 | 22,439 | ||||
2009 | 2030 | 147,358 | 2030 | 147,358 | ||||
2010 | 130 | 8,208 | 130 | 8,208 | ||||
2011 | 100 | 7,382 | 100 | 7,382 | ||||
2012 | 93 | 11,833 | 65 | 4158 | 158 | 15,991 | ||
2013 | 1,906 | 126,340 | 76 | 12,288 | 6 | 4,300 | 1,988 | 142,928 |
2014 | 880 | 80322 | 51 | 4913 | 11 | 1018 | 942 | 86,253 |
2015 | 216 | 23450 | 47 | 4118 | 26 | 2168 | 289 | 29,736 |
2016 | 509 | 29392 | 11 | 565 | 0 | 0 | 520 | 29,957 |
JUMLA | 3,511 | 259,504 | 4,169 | 284,622 | 108 | 11,644 | 7,788 | 555,770 |
- MCHANGO WA VIJANA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
- Kueneza ujumbe wa kutokomeza rushwa kwa jamii kwa kuelimisha wengine kuhusu rushwa, athari zake na namna ya kupambana nayo.
- Kushiriki katika kazi mbalimbali za uelimishaji zinaandaliwa na kuendeshwa kwa ajili ya kuwajengea vijana ufahamu na ujasiri wa kupambana na rushwa.
- Kukataa kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwemo kutoa au kupokea rushwa.
- Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika ofisi za TAKUKURU zilizo karibu au kwa kupiga simu ya bure namba 113 au kwa vyombo vingine vya dola na viongozi wanaohusika. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007
- Kujifunza na kuelewa haki na wajibu wa kila mwananchi pamoja na kuijua katiba ya nchi.
- Kuzingatia maadili na kuwa mzalendo kwakuwa mtu anapoipenda nchi yake kwa dhati atakuwa mstari wa mbele kutetea haki na kuipigania kwa namna yoyote.
- Kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na vyombo vingine vya dola na kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya rushwa kwakuwa mara nyingi TAKUKURU imekuwa ikishindwa kufikia malengo kutokana na wananchi kutotaka kutoa ushirikiano.