JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

Dira Dhima Yetu

Dira Yetu

Dira ya Taasisi ni kuwa chombo bora kinachofanya kazi zake kwa ufanisi na utimilifu huku kikiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025.

Dhima Yetu

Dhima ya Taasisi ni kuzuia na kupambana na rushwa kupitia uelimishaji umma, kuzuia, utambuzi, uchunguzi na mashtaka, na kwa kuwashirikisha wadau ili kuifanya rushwa itambulike kuwa ina madhara makubwa na isiyo na manufaa kwa jamii.

Dhima ya Idara ya Uchunguzi

Dhima ya Idara ya Uchunguzi ni Kubaini, kuchunguza na kuendesha mashtaka ya vitendo vya rushwa na vile vilivyo na mwelekeo wa rushwa

Dhima ya Idara ya Elimu kwa Umma

Dhima ya idara ya elimu kwa umma ni kuishirikisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa.

Dhima ya Idara ya Utafiti na Udhibiti

Dhima ya Idara ya Utafiti na Udhibiti ni Kuzuia vitendo vya rushwa kupitia uimarishaji wa mifumo katika sekita za umma na binafsi

Dhima ya Idara ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini

Dhima ya Idara ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini ni kuiwezesha Tasisi kuwa na mifumo sanifu na thabiti ya mipango,ufuatiliaji,bajeti, na tathimini katika ngazi zote za utekelezaji

Dhima ya Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

Dhima ya Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu ni kuipatia Taasisi mahitaji yake ya watumishi wenye sifa na vitu vingine kwa wakati na sehemu sahihi.