Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kishapu, mkoa wa Shinyanga leo tarehe 09, Oktoba, 2019 itamfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Shinyanga Ndg. BENJAMIN CHARLES MHANGWA ambaye ni Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Kishapu kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007. Soma zaidi