Dkt. Hoseah achaguliwa tena kuwa Mjumbe wa AU-ABC

au hoseah

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt. Edward Hoseah amechaguliwa tena kuwa Mjumbe wa       Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Nchi za Umoja wa Afrika (The African Union Advisory Board on Corruption) kuanzia Januari 2013. Uchaguzi huu umefanyika katika Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama, uliofanyika Januari 28, 2013 Mjini Addis Ababa – Ethiopia.

Hii ni mara ya pili ambapo Dkt. Hoseah anachaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi hii ambayo pamoja na mambo mengine jukumu lake kuu ni kushauri na kusimamia masuala ya Rushwa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Makao Makuu ya Bodi hii yapo Jijini Arusha – Tanzania.

Dkt Hoseah alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mjumbe wa Bodi hiyo katika uchaguzi uliofanywa Januari 29, 2011 na alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na kuiongoza Bodi hii kwa kipindi cha mwaka mmoja. Wajumbe wengine wa Bodi hii ni kutoka nchi za Ethiopia, Côte d’Ivoire, Ghana, Togo, Burundi, Libya, Mali, Benin, Congo na Nigeria. Baada ya muda kutafanyika uchaguzi mwingine ambapo atachaguliwa Mwenyekiti wa Bodi kutokana na wajumbe waliopo.