DKT HOSEAH – RAIS WA EAAACA KWA MARA NYINGINE TENA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Dkt. Edward G. Hoseah, amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki (East African Association of Anti-Corruption Authorities- EAAACA).

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumanne tarehe 29/09/2015 jijini Entebe – Uganda, katika Mkutano Mkuu wa 8 wa shirikisho hilo ulioanza leo.

Hii ni mara ya pili kwa Dkt Hoseah kuchaguliwa kushika wadhifa huo kwani yeye ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza wa shirikisho hilo lililoanzishwa mwaka 2007.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwake, Dkt Hoseah amesema katika kipindi cha uongozi wake kama Rais wa EAAACA (2015 -2017) atatoa kipaumbele katika kutekeleza yafuatayo:

 1. Kuweka mikakati michache inayotekelezeka ikiwemo kufanya tafiti za kuziba mianya ya rushwa katika mifumo mbalimbali ya Taasisi katika za nchi za Afrika Mashariki.
 1. Kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki na kuongeza jitihada za kuhakikisha EAAACA inajumuishwa katika Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (East African Community).

Shirikisho hilo linalojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, liliundwa rasmi Septemba 28, 2007, ambapo viongozi wa TAKUKURU (Tanzania), IG (Uganda) na KACC (Kenya) - ambao ndio waanzilishi, walisaini azimio la kuwa na Ushirikiano wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki.

Azimio hilo lilipewa jina la ‘AZIMIO LA KAMPALA’ na lilitamka kwamba:

 • Taasisi hizi zinarejea dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya kazi pamoja katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa.
 • Taasisi hizi zinatambua kuwa rushwa inaweza kuharibu ufanisi wa kiutendaji wa jamii yoyote, inahatarisha demokrasia, ukuaji wa uchumi na utawala wa sheria. Kwa msingi huu, Taasisi hizi zinaendelea kutilia mkazo kuundwa kwa EAAACA kama jukwaa la kubadilishana taarifa, uzoefu na kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa lengo la kuzuia na kupambana na rushwa katika sura zake zote.
 • Taasisi hizi zinatambua kuwa jukumu la kupambana na rushwa ni la kila mtu katika kila jamii na kwamba mapambano haya yanahusisha ulinzi na uimarishaji wa maadili katika jamii zote.
 • Uamuzi wa kuingia katika makubaliano haya na kuundwa kwa Ushirikiano huu ni ishara ya kweli ya dhamira ya kila moja ya Taasisi hizi katika kutokomeza rushwa.

Kuundwa kwa EAACA ni ishara ya wazi ya dhamira ya viongozi wakuu wa taasisi hizi katika kutekeleza kwa mafanikio jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa katika nchi zao. Hatua hii pia, kama inavyojieleza katika tamko hilo, inazidi kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kila mwanajamii na mataifa katika kukabiliana na tatizo la rushwa duniani.

Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 8 wa EAAACA inasema ‘Uimarishaji wa jitihada za kuzuia na kupambana na Rushwa katika nchi za Afrika Mashariki' na mkutano ujao wa mwaka, umepangwa kufanyika Tanzania mwaka 2016.

Imetolewa na Doreen J. Kapwani, Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Jumanne tarehe 29/10/2015

Dk. Hoseah achaguliwa kuwa Rais EAAACA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dk. Edward G. Hoseah, amechaguliwa kuwa Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki (East African Association of Anti-Corruption Authorities- EAAACA) kuanzia Februari 15, 2008.

Uchaguzi huo ulifanyika katika Mkutano wa kwanza wa Mwaka wa shirikisho hilo linalojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, uliofanyika mjini Zanzibar jana.

Viongozi wengine waliochaguliwa katika mkutano huo na nyadhifa zao kwenye mabano ni Inspekta Jenerali wa Serikali wa Taasisi kama hii ya nchini Uganda inayoitwa Inspectorate of Government of Uganda (IGG)- Jaji Faith Mwondha (Makamu wa Rais); Mkurugenzi wa Kanuni za Maadili ya Uongozi wa IGG -Bi Susan Bisharira (Katibu Mkuu); Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Anti Corruption Commission (KACC) Jaji Aaron Ringera (Mjumbe);Jean Bosco Butisa kutoka Burundi Special Brigade (Mjumbe) na Dk. Tito Rutamelira kutoka Rwanda (Mjumbe). Uongozi huu utadumu kwa kipindi cha miaka miwili ambapo utafanyika tena uchaguzi mwingine.

Shirikisho hili (EAAACA) liliundwa rasmi Septemba 28, 2007, ambapo viongozi wa TAKUKURU, IG na KACC (ambao ndio waanzilishi), walisaini azimio la kuwa na Ushirikiano wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki. Azimio hilo lilipewa jina la ‘AZIMIO LA KAMPALA’ na linasema kwamba:

 • Taasisi hizi zinarejea dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya kazi pamoja katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa.
 • Taasisi hizi zinatambua kuwa rushwa inaweza kuharibu ufanisi wa kiutendaji wa jamii yoyote, inahatarisha demokrasia, ukuaji wa uchumi na utawala wa sheria. Kwa msingi huu, Taasisi hizi zinaendelea kutilia mkazo kuundwa kwa EAACA kama jukwaa la kubadilishana taarifa, uzoefu na kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa lengo la kuzuia na kupambana na rushwa katika sura zake zote.
 • Taasisi hizi zinatambua kuwa jukumu la kupambana na rushwa ni la kila mtu katika kila jamii na kwamba mapambano haya yanahusisha ulinzi na uimarishaji wa maadili katika jamii zote.
 • Uamuzi wa kuingia katika makubaliano haya na kuundwa kwa Ushirikiano huu ni ishara ya kweli ya dhamira ya kila moja ya Taasisi hizi katika kutokomeza rushwa.
 • Katika uwanda wa ushirikiano huu, viongozi wakuu wa EAACA:
 1. Wanadhihirisha tena dhamira zao za kuzuia na kupambana na rushwa na wanatambua umuhimu wa kusaini makubaliano haya.
 2. Wanazishauri Serikali kutokumbatia walarushwa, mali iliyopatikana isivyo halali, na uwekezaji unaotokana na fedha chafu katika nchi zao.
 3. Wanahimiza ushirikiano katika kurejesha wahalifu katika nchi zao, katika masuala ya kisheria, kurejesha mali na fedha zilizopatikana kwa rushwa na katika msaada wa kiufundi.
 4. Wanahimiza kanuni ya kutoivumilia rushwa.

Kuundwa kwa EAACA ni ishara wazi ya dhamira ya viongozi wakuu wa taasisi hizi katika kutekeleza kwa mafanikio jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa katika nchi zao. Hatua hii pia, kama inavyojieleza katika tamko hilo, inazidi kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kila mwanajamii na mataifa katika kukabiliana na tatizo la rushwa duniani.

Leo hii kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, rushwa inazidi kuwa tatizo mtambuko kati ya nchi na nchi na hivyo la kidunia na linalohitaji ushirikiano wa kila mtu ili kulidhibiti. Kutokana na makubaliano haya hakutakuwa na nchi au eneo ambalo mlarushwa ataweza kukimbilia ndani ya Afrika Mashariki kwa maana ya kwamba mtuhumiwa hataweza kutenda kosa katika nchi mojawapo na kukimbilia katika nchi nyingine akidhani atakuwa salama. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu; Jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa ni la kila mmoja wetu, tushirikiane!

Imetolewa na Idara ya Elimu kwa Umma, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Makao Makuu, Dar es Salaam, Februari 16, 2008.

EAAACA Holds its Third Annual General Meeting

The East African Anti-Corruption Authorities (EAAACA) recently held its Third Annual General Meeting in Bujumbura, the capital city of the Republic of Burundi. The meeting was attended by the heads and acting heads of the five anti-corruption authorities forming the association, namely the Special Anti-Corruption Brigade of Burundi (SACB), which hosted the meeting, Kenya Anti-Corruption Commission (KACC), the Office of Ombudsman of Rwanda, the Inspectorate of Government of Uganda, and the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) of Tanzania, the current president of the Association.

IGG visits PCCB

                                                                                                                                                                                                                                                                                          PRESS RELEASE

August 26-28, 2007, the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) hosted a delegation from the Inspectorate of Government of Uganda (IGG), an institution that performs similar functions as the PCCB. The aim of the IGG visit was to share work experiences and to lay a foundation for mutual cooperation between the two parties in the prevention and combating of corruption in Uganda and Tanzania.

The four man delegation was headed by Hon. Justice Faith Mwondha who is the Inspector General of the IGG. The other delegates were Ms Susan Bisharira who is the Director of Leadership Code, Mr. Rwezeera Jossy Jules, Director of Education and Prevention of Corruption and Mr. Kasujja Vincent who is a Technical Assistant for Civil Litigation.

While in Tanzania, Justice Mwondha and Ms Susan visited the PCCB Head Quarters and met with the PCCB Director General, Mr. Edward Hoseah and other Directorates’ Heads. They also visited the Office of the Director of Public Prosecution (DPP), the Ethics Secretariat and office of the Uganda High Commission to Tanzania. They flew back to Uganda via Kenya on September 28, 2007.

The meeting between the IGG and the PCCB was fruitful for both parties whereby despite the sharing of experiences, the IGG and the PCCB signed a four years Memorandum of Understandingwith the objective of preventing and combating corruption in Uganda and Tanzania.

In principle, the IGG and the PCCB have agreed to cooperate in the following areas:

 • Mutual assistance in investigations and prosecution, identification, tracing, freezing, seizure and confiscation of property, instruments or proceeds obtained or derived from corruption.
 • Mutual assistance in training, expertise, attachments and information technology networking to strengthen and develop the institutions.
 • Exchange of information on corruption with a view of developing a common understanding of corruption and sharing information on best practices to prevent and combat corruption.
 • Exchange of delegations once a year to share experiences and expertise.

The IGG and the PCCB shall meet once every year to review the progress of the cooperation and to work out ways of improving the same.

The August IGG visit in Tanzania and Kenya has continued to be of benefit to the three countries with the holding of a meeting in Kampala on September 28 2007. This meeting was attended by Heads of the three countries’ anti-corruption authorities namely Justice Mwondha (Uganda), Justice Aaron Ringera of the Kenya Anti-Corruption Bureau (KACC) and Mr. Hoseah (Tanzania).

On this date, September 28, 2007, the three Heads, on behalf of their Governments signed a declaration for the formation of the East African Association of Anti-Corruption Authorities- EAACA). This Kampala Declaration states that:

 • The IGG, KACC and the PCCB renew their commitment to continue cooperating and working together towards the common objective of preventing and fighting corruption.
 • The parties acknowledge that corruption can destroy the efficient functioning of any society, threatens democracy, economic growth and the rule of law. For this reason, the parties underscore the formation of the East African Association of Anti-Corruption Authorities (EAACA) as an effective platform for the exchange of information, experiences and promotion of international cooperation aimed at combating corruption in all its manifestations.
 • The parties believe that fighting corruption is the business of everyone throughout every society and that this fight involves the defence and strengthening of ethical values in all societies.
 • The willingness to enter into this agreement and formation of this Association is a true test of each individual party’s commitment o the elimination of corruption.  
 • Within the scope of this Association, the Heads of the three EAACA:
 1. Re-affirm their commitment to the prevention and the combating of corruption and recognize the importance by signing the Agreement.
 2. The parties encourage Governments to deny safe haven to corrupt persons, ill-gotten wealth, and investment of tainted money in their countries.
 3. The parties promote cooperation on extradition, mutual legal assistance, asset recovery and return of the proceeds of corruption and technical assistance.
 4. The parties promote the principle of zero tolerance against corruption.

The August IGG visit to Tanzania and Kenya and eventually the formation of the EAACA through the signing of the September 28, 2007 Kampala Declaration is a vivid willingness of the Heads of the IGG, the KACC and the PCCB and their respective organizations in the successful implementation of the organizations’ responsibility of preventing and combating corruption. This milestone move, as stated in the declaration, further reaffirms the importance of every individual and every nation in the curbing of corruption in the world.

To date, with development in science and technology, corruption further becomes a transnational and thus a global problem calling for the participation of every individual to curb the scourge. Together we can fight corruption; the noble duty to prevent and combat corruption is of every individual, let us cooperate!

Issued by the Directorate of Community Education, the Prevention and Combating of Corruption Bureau Head Quarters,

October 4, 2007.