HARBINDER SING SETHI NA JAMES RUGEMARILA WAPANDISHWA KIZIMBANI

Na Mussa Misalaba

Watuhumiwa wawili wa sakata la uchotaji wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow wamepandishwa kizimbani Juni 19, 2017 wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali mabilioni ya fedha.

Waliofikishwa mahakamani ni Mwenyekiti Mtendaji wa Power African Power Solution Ltd, Harbinder Singh (59) na Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing James Buchard Rugemalila (71).

Washtakiwa walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, Huruma Shaidi, na kusomewa mashtaka ambayo hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi na kutoa maamuzi ya dhamana.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili wa Serikali Paul Kadushi  aliyesoma mashtaka, na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Joseph Kiula.

Read more ...

Tanzania yachaguliwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika (AACAA)

Na Mussa Misalaba

Tanzania imechaguliwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mamlaka za Kumpambana na Rushwa Afrika (Africa Anti – Corruption Authorities  Association - AACAA)  katika Mkutano Mkuu wa pili wa Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika  uliofanyika  tarehe 25 – 28 Aprili, 2017 jijini Brazaville , Jamhuri ya Congo.

Katika uchaguzi huo Tanzania ilichaguliwa kuwakilisha nchi za ukanda wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na uchaguzi huo ulifanyika kufuatia kumalizika muda wa uongozi wa awali uliochaguliwa katika mkutano Mkuu wa pili uliofanyika kati ya tarehe 15 – 19 Septemba Accra Ghana.

Nchi zingine ambazo zilichaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya AACAA kwa kipindi cha miaka mitatu na kanda zake ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Afrika ya Kati), Niger (Afrika Magharibi, Uganda (Afrika Mashariki).

Read more ...

TAKUKURU YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA MAFANIKIO

Na Mussa Misalaba

TAKUKURU imepongezwa na gazeti la Habari leo kutokana na kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio na kwa kuzingatia maagizo ya Rais John Pombe Magufuli katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 unaomalizika.

Kupitia toleo lake Namba 03774 la Aprili 20, 2017 ukurasa wa 6 gazeti la Habari Leo limeipongeza TAKUKURU kwa kuokoa zaidi ya bilioni 12.3 ambapo Sh. milioni 912 ni za mishahara hewa, Sh.bilioni 8.3 zilitokana na ukwepaji wa ushuru kupitia mfumo wa kielektroniki wa EFD, Sh.bilioni 2.6 kutokana na ubadhirifu na kiasi kingine cha Sh.milioni 794.18 kiliokolewa katika maeneo mengine.

Aidha, gazeti hili limeipongeza TAKUKURU kwa kufanya vizuri katika uendeshaji wa kesi mahakamani, kuwezesha kutaifishwa kwa mali za washtakiwa wa rushwa, na udhibiti wa mianya ya rushwa katika mifumo ya hati za kusafiria na sheria na kanuni za uanzishwaji na usimamizi wa maduka ya dawa muhimu za binadamu.

Hizi ni fedha nyingi ambazo zitasaidia serikali katika baadhi ya maeneo muhimu.Tunaamini kupatikana kwa fedha hizo kunaongeza hali pia kwa taasisi nyingine kuiga mfano”,limeandika gazeti.

Tunalipongeza gazeti hili kwa kuona na kuthamini mchango wa TAKUKURU katika kukabiliana na uharifu nchini katika kipindi hiki ambacho serikali inapambana kudhibiti mapato yake yanayoishia mfukoni mwa watu wasiowaaminifu na tunaamini pongezi hizi ni chachu kwetu kuweza kufanya vizuri zaidi kwa mwaka wa fedha ujao.

Fungua Kiambatanishi

MBUNGE ATAKA MAFISADI WAFUNGWE MINYORORO MAKABURINI


Na John Kabale, Dodoma,

Mbunge wa Nkasi (CCM) Mhe. Ally  Kessy ameonesha kukerwa na mafisadi na wezi wa mali ya umma wakati akichangia hotuba iliyowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2017/2018 na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017 Aprili 11, 2017.

Read more ...

TAKUKURU yakabidhi kwa Rais taarifa ya utendaji kwa mwaka 2015/2016

Murugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola akikabidhi kwa Rais John Pombe Magufuri taarifa ya Utendaji wa ofisi kwa Mwaka 2015/2016 Ikulu Dar-es salaam Aprili 11, 2017
Murugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola akitoa maelezo mafupi kwa Rais John Pombe Magufuri mara baada ya kukabidhi taarifa ya Utendaji wa ofisi kwa Mwaka 2015/2016 Ikulu Dar-es salaam Aprili 11, 2017

Subcategories