Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

 

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam Mheshimiwa Simba na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Makao Makuu Bw. Joseph Kiula.

Mwendesha Mashitaka aliieleza mahakama kuwa, mnamo tarehe 18/10/2009 na tarehe 27/10/2009 washtakiwa wakiwa na nia ya kudanganya, waligushi invoice namba 346 na namba 0221 zikionyesha kuwa Chama Cha Ushirika Shinyanga (1984) kimesambaza tani 1000 za pamba zenye thamani ya Tsh 145,000,000/= (milioni mia moja arobaini na tano).

Katika kosa jingine, mshatakiwa Adam Yusuphu (Monitoring and Supervision Officer of Tanzania Investment Bank), anashtakiwa kwa kosa la Uchepushaji wa fedha kiasi hicho cha tsh 145,000,000/= kwenda katika akaunti ya kampuni ya Simon Group Limited. Kesi imepangwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH) tarehe 18.8.2015