MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA MWAKA 2014 YAFANA DODOMA.

  • Bi. Emma Kuhanga angoza watumishi kujitolea sadaka kwa watoto yatima na wasio jiweza.
  • Asema palipo na Upendo, Amani na Matumaini, Rushwa haina nafasi.
  • Masista wa Shirika la Ursuline waipongeza na kuishukuru TAKUKURU Dodoma kwa wema na upendo wao.
  • Sista Aurela Kyara atoa wito kwa watu wote wenye upendo wa dhati kujitolea kuwasaidia yatima na wasio jiweza.

Na Colman Lupembe - Dodoma.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika mkoani Dodoma tarehe 10/12/2014 yalifana na yalisaidia kuikumbusha jamii wajibu wao kuwasaidia yatima na wasiojiweza, kwani ni ukweli usiopingika kuwa palipo na Upendo, Amani na Matumaini, Rushwa haina nafasi kamwe.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka 2014 ni “Vunja Mnyororo wa Rushwa” Akizungumzia kauli mbiu hiyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bi. Emma Kuhanga aliwasihi masista na watumishi wote wa kituo cha kulelea yatima na wasio jiweza cha Nyumba ya Matumaini, kuthamini michango mbalibali kutoka kwa wafadhili na kuhakikisha kuwa kweli inawafikia walengwa kama inavyo kusudiwa. Bi. Emma Kuhanga alisisitiza kuwa palipo na Upendo, Amani na Matumaini mara zote Rushwa haina nafasi na kamwe mahali hapo matendo ya Rushwa hayatasikika. Bi Emma Kuhanga alisisitiza kuwa Rushwa mara zote ni adui wa haki, na aliwapongeza Masista na watumishi wote wa Kituo cha Nyumba ya Matumaini kwa juhudi kubwa wazifanyazo katika kubeba jukumu zito la kuwalea watoto yatima na wasio jiweza katika kituo chao kwa muda wote.

Misaada iliyotolewa na watumishi wa TAKUKURU ni Sukari kilo 50, Mafuta ya kula lita 10, Sabuni ya unga kilo 15, Sabuni za miche katoni 5, Dawa za Meno katoni 3, unga wa mahindi kilo 50, pamoja na nguo na viatu vyote kwa pamoja vilifikia thamani ya Shilingi 500,000/=.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa kituo cha Nyumba ya matumaini Sista Aurela Kyara aliishukuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma kwa Misaada yao waliyoitoa kwa watoto yatima na wasio jiweza na kuahidi kuitumia kwa mujibu wa mahitaji ya walengwa na kama ilivyo kusudiwa na kuahidi kuzingatia maadili wakati wa kuzitumia.                                 

“Kituo chetu kina mahitaji mengi na ambayo yana gharama kubwa, msaada wenu utasaidia kutoa ahueni na kuboresha hali ya utoaji huduma kwa watoto yatima na wasio jiweza ” alisema Sista Kyara.

Aidha, Sista Kyara alitoa wito kwa Taasisi nyingine kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia watoto yatima na wasio jiweza kwani jukumu la kuwalea watoto hao ni la kwetu sote.

Pamoja na kutoa misaada, Bi Emma Kuhanga alitumia fursa hiyo kuwapa watumishi wa nyumba ya matumaini na watoto yatima na wasio jiweza elimu ya rushwa na kuwataka washiriki katika mapambano dhidi ya rushwa. Vijarida na vipeperushi kadhaa pia viligawiwa.

Wakati huo huo TAKUKURU Mkoa Dodoma ilishiriki katika kipindi cha “ana kwa ana” kupitia Redio Dodoma FM 98.4 MHZ hapo tarehe 4 Desemba, 2014 ambapo Afisa wa Dawati la Elimu kwa Umma Bw. Colman Lupembe alitoa taarifa juu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambapo aliwataka wasikilizaji kuhakikisha maadili yanazingatiwa katika kila sekta kwani “palipo na maadili rushwa hutoweka”.

TAKURURU yapongezwa katika maonyesho ya Sabasaba

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt. Edward Hoseah amechaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Nchi za Umoja wa Afrika (African Union Advisory Board on Corruption) kuanzia Januari 2013. Uchaguzi huu umefanyika katika Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama, uliofanyika Januari 28, 2013 Mjini Addis Ababa – Ethiopia.

Hii ni mara ya pili ambapo Dkt. Hoseah anachaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi hii ambayo pamoja na mambo mengine jukumu lake kuu ni kushauri na kusimamia masuala ya Rushwa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Dkt Hoseah alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mjumbe wa Bodi hiyo katika uchaguzi uliofanywa Januari 29, 2011 na alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na kuiongoza Bodi hii kwa kipindi cha mwaka mmoja. Wajumbe wengine wa Bodi hii ni kutoka nchi za Ethiopia, Côte d’Ivoire, Ghana, Togo, Burundi, Libya, Mali, Benin, Congo na Nigeria. Baada ya muda kutafanyika uchaguzi mwingine ambapo atachaguliwa Mwenyekiti wa Bodi kutokana na wajumbe waliopo.

TAKUKURU Kagera yashiriki maonyesho ya sabasaba

Julai 4-7, 2010 ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Kagera ilishiriki maonyesho ya SabaSaba yaliyoandaliwa na ‘Kagera Agricultural and Industrial Development Promotion’ (KAIDEP).  Maonyesho hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa CCM - Bukoba Mjini.

Shughuli za uelimishaji zilizofanyika ni pamoja na kuelimisha wananchi waliotembelea banda, kupokea taarifa, kero, maoni na ushauri kutoka kwa wananchi na kuzifanyia kazi. Pia ilihusisha kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi na kugawa machapisho yenye ujumbe dhidi ya rushwa.

TAKUKURU ilitumia maonyesho hayo kuwaelimisha wananchi mikakati iliyojiwekea kuzuia rushwa kuelekea uchaguzi mkuu. Mikakati hiyo ni pamoja na kuwaelimisha wananchi kwa njia ya mikutano ya hadhara, vipindi vya redio na televisheni, maigizo, matangazo na mabango yenye ujumbe wa kukemea vitendo vya rushwa.  Mkakati mwingine ni kuwachunguza wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya rushwa.

Vilevile, TAKUKURU ilitumia maonyesho hayo kuwahimiza wananchi kupiga kura kuchagua viongozi waadilifu ambao hawatajihusisha na vitendo vya rushwa na wananchi wenyewe kutojihusisha na vitendo vya rushwa. Pia wananchi wamahimizwa kushiriki  mapambano dhidi ya rushwa kwani si ya TAKUKURU peke yake, ni ya kila mmoja kwa nafasi aliyonayo. Ni kwa ushirikiano kati ya wananchi na Serikali  rushwa inaweza kupungua kama si kuisha kabisa.

Kwa upande mwingine, wananchi walishauri TAKUKURU kutembelea mara kwa mara maeneo yanayolalamikiwa sana kwa vitendo vya rushwa kama vile Mahakama, Hospitali, vizuizi vya  barabarani na ofisi za Ardhi  kwa lengo la  kuelimisha na kudhubiti vitendo vya rushwa maeneo hayo.

Elimu dhidi ya rushwa iliyotolewa kwa wananchi katika maonyesho ya SabaSaba ni ya muhimu sana kwani wameongezewa ufahamu juu ya rushwa na madhara yake kwa ujumla na hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Ni matarajio ya TAKUKURU kuwa wananchi wameelimika hivyo hawatajihusisha na vitendo vya rushwa na watendelea kuunga mkono juhudi za  Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.

Jumla ya wananchi 768 walitembelea banda la TAKUKURU na kuelimishwa. Pia machapisho 1,505 yenye ujumbe dhidi rushwa yaligawiwa ili wananchi waendelee kujipatia elimu kwa kuyasoma.

TAKUKURU yaendesha shindano la nyimbo mikoani

Dhima ya Idara ya Elimu kwa Umma ya TAKUKURU  ni kushirikisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa. Kwa kutambua umuhimu wa sanaa, Machi 2010 TAKUKURU ilishirikisha Vikundi 314 toka mikoa yote ya Tanzania Bara katika  shindano la nyimbo lililolenga kuelimisha jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu.

 Shindano hilo lilianzia katika ngazi ya wilaya na hatimaye mkoa  kwa kushirikisha  vikundi vya  kwaya.

Vigezo viliyotumika katika shindano ni pamoja na ujumbe uliowasilishwa, muda wa wimbo,  matumizi ya jukwaa, utoaji wa sauti, uwiano wa sauti na matamshi na uwasilishaji.

 Ili kufanikisha shindano hilo, TAKUKURU ilishirikiana na Maafisa Utamaduni wa Mkoa na Wilaya katika kupata washindi wa wilaya na mikoa kulingana na vigezo vilivyowekwa.

Washindi wa ngazi ya Mikoa walikuwa wafuatao;

Tourism(Arusha), Sakis Star  (Dodoma), Upendo Group (Ilala), S.P.W  Youth Talents(Iringa), Utatu (Kagera), Kasulu Theatre Art Group KATG (Kigoma), Kilimanjaro Sanaa Group (Kilimanjaro), Shule ya Sekondari makongo(Kinondoni), Lindi Revolution (Lindi) Panga (Manyara) Mwembesono Thearte Group (Morogoro), Kwaya ya Safina (Mtwara), Kwaya ya Mtakatifu Fransisco Nyakahoja (Mwanza) Vitali Maembe (Pwani), TAG-VCC (Rukwa),Masumini Mbinga (Ruvuma), KKKT – Meatu (Shinyanga),St. Michael Choir (Singida),

Magereza Sanaa Group (Tabora),Kwaya ya Mapinduzi (Tanga) na Miburani Sekondari (Temeke).

Shindano hilo kwa ngazi ya Taifa linategemea kufanyika mwezi Agosti, 2010 ambapo mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya fedha taslimu pamoja na ufadhili wa kurekodi nyimbo.

SAFAC Meeting

UKURU Dkt. Edward Hoseah aliendesha mafunzo kwa viongozi wa dini, wakuu wa shule za sekondari, walimu walezi na viongoz