UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO – MONDULI
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Monduli, Bw Ismail Bukuku (Mwenye shati jeupe), amesisitiza umuhimu wa Kamati ya Ujenzi na viongozi wa serikali za vijiji katika kusimamia miradi ya maendeleo. Msisitizo huo aliutoa katika Kijiji cha Loolera wakati akifuatilia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa choo cha shule shikizi ya Loolera ambao ujenzi wake umekuwa ukisuasua. TAKUKURU Monduli Januari 23, 2023.