TAKUKURU KILIMANJARO YAELIMISHA WANACHUO MWEKA

TAKUKURU KILIMANJARO YAELIMISHA WANACHUO MWEKA

“Ukiombwa rushwa ya ngono toa taarifa kwa TAKUKURU ili mwombaji wa rushwa ya ngono ashughulikiwe na kuondolewa kwenye nafasi yake. Hii itawezesha mchakato wa nafasi uliyoomba wakati wa kujiunga na chuo au usahihishaji wa mitihani yako ufanywe kwa haki na watu ambao ni waadilifu”. Hayo yalisemwa na Mkuu wa TAKUKURU (M) Kilimanjaro, Bi. Frida Wikes (Aliyesimama), Disemba 3, 2022.

WATOTO WA KANISA LA SABATO WAELIMISHWA

WATOTO WA KANISA LA SABATO WAELIMISHWA

Elimu ya kukuza maadili kwa watoto wa Kanisa la Sabato la Dodoma Kati wenye umri kati ya mwaka 1 hadi miaka 18 imetolewa ikiwa ni kuelekea kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, ambayo itaadhimishwa Desemba 10, 2022. Mmoja wa watoto hao amesema “…..rushwa ni dhambi hivyo anayetoa au kupokea rushwa sio mtoto wa Mungu  bali ni mtoto wa shetani ….” TAKUKURU Dodoma, Desemba 3, 2022