Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP. Salum Rashid Hamduni, alipomtembelea leo Mei 16, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP. Salum Rashid Hamduni akimkabidhi Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU wa mwaka 2020/2021 kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Na. 11 ya mwaka 2007. Taarifa hiyo ilikabidhiwa leo tarehe 30 Machi, 2022, Ikulu – Chamwino Dodoma.