JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

Kituo cha huduma kwa mteja

UTANGULIZI

Ofisi ilianza kazi rasmi tarehe 24.05.2016 baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan. Ofisi ipo Makao Makuu ya TAKUKURU – Upanga jijini dar-es-Salaam na inafanya kazi masaa 24. Jukumu kuu la ofisi hii ni kupokea na kujibu simu, sms pamoja na USSD zinazotumwa na wananchi BURE kuja TAKUKURU.

Mitandao iliyounganishwa na huduma hii ni AIRTEL; HALOTEL; TIGO; TTCL; VODACOM na ZANTEL ambapo huduma zinazotolewa ni za kupiga  SIMU – 113; Kutoa taarifa za rushwa kwa kupiga *113# na kutuma maoni au kuuliza maswali kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kupitia 113

Vilevile, simu nambari 113 za mitandao ya AIRTEL, HALOTEL na TIGO imeunganishwa moja kwa moja kwenda katika ofisi za TAKUKURU Mikoa husika.

Kwa taarifa zaidi tazama TAARIFA ZA KILA MWEZI.

 

TAARIFA YA MEI – JUNI 2016

TAARIFA YA JULAI 2016

TAARIFA YA AGOSTI 2016

TAARIFA YA SEPTEMBA 2016

TAARIFA YA OKTOBA 2016