-
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP. Salum Rashid Hamduni akimkabidhi Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU wa mwaka 2020/2021 kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Na. 11 ya mwaka 2007. Taarifa hiyo ilikabidhiwa leo tarehe 30 Machi, 2022, Ikulu – Chamwino Dodoma.