JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

WAZIRI MCHENGERWA AFANYA KIKAO KAZI NA VIONGOZI WA TAKUKURU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Mei 19, 2021 amefanya kikao kazi na viongozi wakuu wa TAKUKURU na kutoa maelekezo ya namna ya kuimarisha utendaji kazi. Kikao kazi hicho kilichofanyika PCCB HOUSE Dar Es Salaam, kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bi Neema Mwakalyelye (ambao wote waliapishwa na Mhe. Rais jana kushika nyadhhifa zao) pamoja na Wakurugenzi na baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi.

Pamoja na mambo mengine, Mhe Waziri ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi, alisisitiza mambo yafuatayo: Utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa TAKUKURU Machi 28, 2021 tulipokabidhi Taarifa ya Utendaji Kazi kwa mwaka 2019/2020; Kazi za TAKUKURU zijielekeze pale ambapo kuna tuhuma za Rushwa, Uhujumu Uchumi pamoja na Ubadhirifu wa mali ya umma; Kutunza siri za watoa taarifa na mashahidi; Kushughulikia malalamiko na madai ya watumishi ikiwa ni pamoja na kuweka mipango ya kuwezesha watumishi kupata mafunzo ya mara kwa mara yatakayoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.