JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

UELIMISHAJI SIKIKA

 

MAFUNZO YA RUSHWA KWA WAGANGA WAFAWIDHI, WENYEVITI NA WAJUMBE WA KAMATI ZA VITUO VYA AFYA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU na Shirika Lisilo la Kiserikali la SIKIKA, wanashirikiana katika kazi ya kuelimisha jamii dhidi ya rushwa. Ushirikiano huu ulianza mwaka 2020, lengo kuu likiwa ni kutoa mafunzo kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati za Vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na wananchi kuhusu madhara ya rushwa katika afya na kuwahamasisha kutoa taarifa za rushwa TAKUKURU kupitia nambari ya dharura 113.
Kwa kuanzia uelimishaji huu ulifanyika wilayani Kondoa (Dodoma) tarehe 26, Novemba 2020 na kufuatiwa na Wilaya ya Simanjiro (Manyara) tarehe 28, Aprili 2021. Aidha kwa mwaka 2021 SIKIKA walikuwa wamepanga uelimishaji ufanyike Wilaya ya Simanjiro na Kasulu lakini kutokana na mafanikio yaliyopatikana, kazi hiyo iliongezewa wigo wa kufikia wilaya kumi zaidi kama zinavyooneshwa kwenye jedwali hapo chini.
Kufikia tarehe 16/6/2021 uelimishaji umeshafanyika katika wilaya nne (Kondoa, Simanjiro, Kiteto na Kilwa)
SIKIKA wamekuwa wakifuatilia taarifa za rushwa katika utoaji wa huduma za afya kwenye vituo vya umma tangu mwaka 2013.

RATIBA YA MAFUNZO KWA KILA WILAYA
NA. MKOA WILAYA JINA LA AFISA MWELIMISHAJI TAREHE
1. Dodoma Mpwapwa Maura Mntambo 23/6/2021

2. Iringa Iringa mjini DitramMhoma 23/6/2021
Kilolo Kaleb Mwenda 25/6/2021

3. Kigoma Kigoma Ujiji Leonida Mushema 24/6/2021
Kasulu Abdul Kapiten 22/6/2021

4. Kilimanjaro Moshi vijijini Lilian Lyimo 25/6/2021
Siha Yohana Marwerwe 23/6/2021

5. Lindi Lindi Justine Maingu 17/6/2021
Kilwa Pius Rugalabamu 15/6/2021

6. Manyara Babati Richard Samila 17/6/2021
Kiteto Emmanuel Manyutwa 15/6/2021