JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

DG TAKUKURU: WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) CP. Salum Rashid Hamduni, amewataka Watumishi wa Umma kote nchini kuzingatia miiko na maadili ya taaluma zao ili kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa.

Akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Juni 17, 2021, CP. Hamduni amesema kila kazi ina miiko na maadili yake, hivyo ni muhimu kwa kila mtumishi kuizingatia.

Akiwa wilayani Kakonko, Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU ameshiriki zoezi la upandaji miti katika haspitali ya wilaya hiyo, kuzungumza na Viongozi wa Watumishi katika idara mbalimbali, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.

Kamishna Hamduni alikuwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma - 2021.