JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

SEMINA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA (USEMI)

Septemba 7, 2021, TAKUKURU iliandaa Semina kwa ajili ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI).

Lengo la Semina hii lilikuwa ni kujengeana uwezo na pia kutekeleza hitaji la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 ambayo inatutaka, pamoja na mambo mengine, kuelimisha umma kwenye makundi mbalimbali.

Semina hii ambayo ilifanyika katika ukumbi wa TAKWIMU jijini Dodoma, ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu, Naibu Mkurugenzi Mkuu pamoja na Wakurugenzi wa TAKUKURU; Mhe. Abdallah Jafari Chaurembo (Mb), ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya USEMI; Mhe. Mohammed Omary Mchengerwa (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni mjumbe wa kamati hii aliyeongozana na Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb) Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu Ofisi Rais – Ikulu na Katibu Mkuu – Utumishi.

Mada kuhusu ‘RUSHWA NA WAJIBU WA WABUNGE KATIKA KUPAMBANA NA RUSHWA’ iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU Mhandisi, Dkt. Emmanuel Kiyabo na kujadiliwa na wajumbe wote.