JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

TAKUKURU NA CHAMA CHA SKAUTI WAENDESHA MAFUNZO

Mafunzo kwa Wawezeshaji ya kuwapitisha katika MWONGOZO WA KUFUNDISHA VIJANA WA SKAUTI KUHUSU KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA yameanza leo Jijini Dodoma. Mafunzo haya yanafanyika kwa ushirikiano kati ya TAKUKURU, Chama cha Skauti Tanzania, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS) na yanawakutanisha Wakuu wa TAKUKURU Mikoa, Maafisa Elimu Mikoa na Makamishna wa Skauti kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara. Viongozi hawa ndiyo watakaokuwa wawezeshaji wa mwongozo huu katika maeneo yao ya kazi. Ufunguzi wa mafunzo utafanyika Septemba 23, 2021 na kuhitimishwa Ijumaa Septemba 24, 2021 na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu (Mb).