JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

TAKUKURU Yaendelea Kukuza Uhusiano Kimataifa Katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa

TAKUKURU kwa kutambua umuhimu wa kushirikiana na wadau ikiwemo Wadau wa Maendeleo, imeendelea kufanya Vikao Kazi kwa lengo la kukuza ushirikiano huo pamoja na kutafuta fursa zaidi katika kuzuia na kupambana na rushwa.

PICHA NA. 1: Mkurugenzi Mkuu CP. Diwani Athumani katika Kikao Kazi na Balozi wa Uswisi Mhe. Florence Tinguely Mattli (Gauni la Blue), Januari 29, 2019 - TAKUKURU Upanga, Dar es Salaam. Mkutano huu ulijadili maboresho ya MoU kati yetu katika Uchunguzi, Utafiti na Urejeshaji wa Mali. Wajumbe wengine ni kutoka International Center for Asset Recovery na Basel Institute of Governance kilichopo nchini Uswiss.  

 

PICHA NA 2:

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi Kassim Ephrem katika Kikao Kazi na Ujumbe kutoka GIZ (Shirika la Maendeleo la Ujerumani). Mkutano huu ulijadili jinsi TAKUKURU inavyoweza kushirikiana na GIZ ambao pia wamekuwa wakitoa msaada kupitia Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki (East African Association of Anti Corruption Authorities - EAAACA) Januari 31, 2019 TAKUKURU, Upanga, Dar es Salaam

 

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi, Kassim Ephrem (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mradi wa Utawala Bora GIZ Tanzania, Dr. Annette Mummert (wa tatu kulia) katika kikao hicho.