JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

African Parliamentarians Network against Corruption (APNAC)

APNAC ni mtandao wa wabunge wa mabunge ya Afrika wenye lengo la kuwahusisha katika mapambano dhidi ya rushwa. Mtandao wa APNAC ulianzishwa mapema Februari 1999 Kampala Uganda kufuatia semina ya wiki moja iliyohusu Bunge na Utawala Bora:Kuelekea agenda Mpya ya Kudhibiti rushwa katika vita dhidi ya rushwa. Semina hii iliandaliwa na Kituo cha Bunge la Kananda kwa ushirikiano na Kamati ya Hesabu ya Bunge la Uganda, Taasisi ya Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza.Wabunge thelathini  toka kila kanda ya Afrika walishiriki.

Washiriki wa semina hii walikubaliana kwa pamoja umuhimu wa wabunge wa Afrika kuwa na ushirikiano katika kubadilishana taarifa, uzoefu, na uelewa katika kuimarisha mabunge katika vita dhidi ya rushwa. Kutokana na sababu hii, APNAC ilianzishwa