JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

Umoja wa Mataifa

UNCAC (United Nations Convention Against Corruption)

Ni Mkataba wa umoja wa mataifa wa kuzuia na kupambana na rushwa   uliosainiwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 9Disemba, 2003  Merida, Mexico. Mkataba huu ulisainiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mtaifa ikiwa ni jitihada za kutambua rushwa ni tatizo la dunia nzima. Mkutano huu ni tukio la kihistoria katika juhudi za  dunia kupambana na rushwa. Zaidi ya nchi 100 zilishiriki katika sherehe hii na ziliahidi kwa dhati kupambana na rushwa. Tangu kipindi hicho wazo hili limeendelea kuungwa mkono na Mamlaka nyingi za Kupambana na Rushwa kutoka nchi mbalimbali , mashirika ya kimataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Madawa na Uhalifu (United Nations Office on Drugs and Crime – UNODC) Viena. Ofisi za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia madawa na uharifu (UN Office on Drugs and Crime – UNODC) zilizoko Viena Austria zinatumika kama sekretariati ya UNCAC. Mkataba huu una vifungu vinavyohusiana na masuala ya uchunguzi, uendeshaji wa mashtaka ya makosa ya rushwa, uzuiaji wa mali, utaifishji na urejeshaji wa mali zilizotokana na makosa ya rushwa. Nchi  165 zimesaini mkataba huu. Tanzania ilisaini mkiataba huu tarehe 9Desemba 2003 na kuridhiwa na UNCAC tarehe 25 Mei 2005. Mkataba huu ni wa aina yake kwa vile:

 • unahusisha nchi nyingi
 • Mkataba unazitaka nchi wanachama kuchukua hatua muhimu ikiwa ni pamoja na kutunga sheria na kuchukua hatua za kiutawala kulingana na misingi muhimu ya sheria zake ili kuhakikisha matakwa ya mkataba huu yanafikiwa.
 • una vipengere vya kuzuia na kuadhibu wahusika wa vitendo vya rushwa
 • Nchi wanachama zinawajibika kusaidiana katika maswala ya uharifu wa kuvuka mpaka.Ushirikiano huu ni pamoja na ukusanyaji na uwasilishaji wa ushahidi mahakamani.Ushirikiano katika makosa ya jinai ni wa lazima lakini kwa upande masuala ya madai ni wa hiari. Aidha, mkataba unazipa haki nchi wanachama kurejeshewa mali ya umma zilizo ibiwa na kutoroshewa nje ya nchi. Nchi nyingi zinazoendelea zinmeridhia mkataba huu kwa sababu hii ya kurejeshewan mali.
 • Kila nchi mwanachama inatakiwa, kwa kadri iwezekanavyo, kuanzisha, kuendeleza au kuboresha programu maalum za mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wake wanaoshughulikia masuala ya kuzuia na kupambana na rushwa.Mafunzo hayo ni pamoja na mbinu za kuzuia, kubaini, kuchunguza, na kudhibiti rushwa.
 • Nchi wanachama zilizoridhia mkataba huu zinalazimika pia kushirikiana katika kuzuia na kupambana na rushwa katika maeneo ya uchunguzi na misaada ya kiufundi ambayo imetafsiriwa kama fedha, raslimali watu, mafunzo, na utafiti.
 •  Mkataba huu unahimiza ushirikishwaji wa wananchi na taasissi zisizo za kiserikali katika michakato ya uwajibikaji na pia uhuru wa kupata habari.
 • Nchi wanachama zinawajibika kuwa na sera za kuzuia rushwa na kuwa na chombo au vyombo vya kuratibu na kusimamia utekelezaji wake.Sera za kuzuia rushwa ambazo zimeainishwa na mkataba huu zinalenga sekta za umma na binafsi ambazo ni pamoja na:
 • Manunuzi ya wazi
 • Usimamizi imara wa fedha
 • Utumishi wa umma ulio na hadhi ikiwa ni pamoja na kujuuzuru pale panapokuwa na maslahi yanayokidhana, umma kupata taarifa bila kizingiti, ukaguzi wa mahesabu na vigezo vingine kwa makampuni binafsi
 • mahakama huru
 • kuishirikisha jamii kikamilifu katika kuzuia na kupambana na rushwa
 • kuchukua hatua za kukabiliana na utakatishaji wa fedha haramu.

Kuona na kusoma  mkataba wa UNCAC bonyeza hapa

Makala ya uchambuzi wa UNCAC

IAACA (International Association of Anti – Corruption Authorities)

Ni Shirikisho huru la Kimataifa, lisilo la kiserikali, lisilo na mlengo wa kisiasa na lisilo na nia ya kupata faida la Mamlaka  mbalimbali za Kupambana na Rushwa. Makao makuu ya IAACA yako Beijing, China. IAACA  ni nyumba ya mamlaka za kupambana na rushwa kama ambavyo Dimitri Vlassis, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alipata kusema kwenye kongamano la 8 la mwaka la IAACA lililofanyika Saint Petersbug, Urusi  kati ya tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba, 2015. Wazo la kuwa na chombo hiki lilitolewa kwenye  Mkutano Mkuu wa  kisiasa uliofanyika kwa ajili ya kusaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa (UNCAC) Merida, Mexco mwezi Desemba, 2003. Mkutano huu ni tukio la kihistoria katika juhudi za  dunia kupambana na rushwa. Zaidi ya nchi 100 zilishiriki katika sherehe hii na ziliahidi kwa dhati kupambana na rushwa. Katika mkutano huu Wawakilishi wengi wa UNCAC walipendekeza kuanzishwa kwa chombo huru cha kimataifa, kisicho na mlengo wa kisiasa na kisicho na nia ya kupata faida ambapo wanachama wake ni Mamlaka za Kupamabana na Rushwa kutoka nchi mbalimbali duniani.

Tangu kipindi hicho wazo hili limeendelea kuungwa mkono na Mamlaka nyingi za Kupambana na Rushwa kutoka nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Madawa na Uhalifu (United Nations Office on Drugs and Crime – UNODC) Viena.

Wakati wa kikao cha majadiliano yasiyo rasmi juu ya uanzishwaji wa shirikisho la kimataifa la mamlaka za kupambana na rushwa kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Viena tarehe 19-20 Aprili, 2006 wawakilishi toka mashirika ya kimataifa na Mamlaka za Kupambana na rushwa  kutoka Argentina, Azerbaijan, Ufaransa, Ujerumani, India, Japan, Korea, Latvia, Malaysia, Namibia, Uholanzi, Pakistan, Romania, Singapore, Afrika Kusini, Uganda, Uingereza, na Marekani pamoja na viongozi wa UNODC walikubaliana na wazo la kuanzishwa kwa IAACA.

IAACA ilianzishwa rasmi Oktoba 22, 2006 jijini Grand Epoch, Beijing nchini China wakati wa Kongamano  na mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Oktoba 22-26, mwaka 2006 kwa msaada mkubwa wa Umoja wa mataifa na ridhaa ya China . Katika lengo lake la kusaidia utekelezaji wa UNCAC, IAACA imeandaa kwa mafanikio matukio mbalimbali kwa lengo la kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja na  Kongamano la mwaka na mkutano mkuu uliofanyika Beijing China  Oktoba 22 hadi 26,2006, semina ya kwanza ilifanyika Guanghou China tarehe 17-26 mwezi Juni, 2007, Kongamano la pili la mwaka na Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 21-24 mwezi Novemba, 2007 Bali Indonesia na Semina ya pili iliyofanyika tarehe 16-19 mwezi Mei, 2008 Chongqing , China. Hadi kufikia tarehe ya kongamano la 8 la IAACA lililofanyika Saint Petersburg, Urusi tarehe 11/2/2015 shirikisho lilikuwa na wanachama wapatao 300 ambao ni pamoja na mamlaka za kupambana na rushwa, mahakama na mamlaka za kusimamia sheria na mashirika ya kupambana na rushwa.

Lengo kuu la IAACA ni kuhimiza utekekelelezaji wenye mafanikio wa mkataba mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya rushwa (UNCAC), kusaidia mamlaka za kupambana na rushwa duniani katika kupambana na rushwa. Kuona na kusoma katiba ya IAACA bonyeza hapa.