JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

MKATABA WA UMOJA WA AFRIKA WA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Mkataba wa umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa  ulipitishwa  mjini Maputo(Msumbiji) tarehe 11 Julai 2003 kupambana na rushwa ya kisiasa iliyokithiri katika bara la afrika. Mkataba huu unawakilisha makubaliano ya kikanda kwa nchi  wanachama wa Umoja wa  Afrika  kuhusu nini nchi hizi   zifanye katika mapambano dhidi ya rushwa hususan maeneo ya mazuio ya rushwa, uhalifu, ushirikiano wa kimataifa na uokoaji mali. Mkataba unajumuisha maeneo mengi ya makosa ya mlungula (ndani na nje ya nchi), uchepushai wa mali za umma, ukuwadi wa mamlaka, mapato haramu,  utakatishaji wa fedha haramu na ufichaji wa mali.

Wajumbe wa Umoja wa Afrika walipisha  Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa uliokubaliwa katika kikao cha pili cha baraza cha umoja huo, kilichofanyika mjini Maputo (Msumbiji), tarehe 11 Julai 2003. Mkataba huu ulianza kufanyakazi tarehe 5 Agusti 2006. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016 nchi zipatazo 37 zilikwisha ridhia mkataba huu.

UTARATIBU WA  UTEKELEZAJI MAJUKUMU

Mkataba umeweka mfumo wa ufuatiliaji na usimamizi ambapo jukumu hili imepewa Bodi ya ushauri wa masuala ya rushwa ndani ya AU. Bodi ina wajumbe 11 wanaoteuliwa na Baraza la Utendaji la AU toka miongoni mwa watalaamu wenye maadili ya hali ya juu, wasio na upendeleo wowote na wenye uwezo wa kuzuia na kupambana na rushwa ambao hupendekezwa na nchi wanachama wa AU.


Katiba ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na Kupambana na Rushwa

Jarida la Haki za Binadamu:Mkataba wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa AU

Nchi za AU zilizosaini na kuridhia Mkataba wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa

 

ITIFAKI YA SADC DHIDI YA RUSHWA

ITIFAKI YA SADC dhidi ya rushwa ilianzishwa na wakuu wa nchi na serikali wanachama wa SADC katika kikao chao cha Agosti14, 2001 kilichofanyika Blantyre, Malawi na hivyo kuwa mkataba wa kwanza na wa aina yake katika ukanda huu. Kuanzishwa kwa Itifiki ya SADC ni kutambua kuwa rushwa imekuwa ni tatizo la dunia nzima bila kusahau ukanda wa Afrika ya Kusini.Wazo la kuwa na chombo cha kupambana na rushwa kusini mwa Afrika lilitolewa kwanza kama Tamko dhidi ya rushwa kwenye kikao cha viongozi wa juu wa SADC kilichofanyika tarehe 23Agosti 1998, Harare Zimbabwe ambapo Sekretariati ilisistiza kwamba Kusini mwa Afrika lazima ichukue hatua thabiti za kupambana na rushwa.ITIFAKI YA SADC dhidi ya rushwa inabainisha na kufafanua aina ya matendo ya rushwa ambayo nchi wanachama zinapaswa kuyatokomeza kupitia hatua mbalimbali zilizobainishwa na itifaki hii ya SADC.

Madhumuni ya itifaki hii ni:

  • kukuza  na kuimarisha, kwa upande wa  kila nchi mwanachama, mifumo inayohusika na kuzuia, kuchunguza, kuaadhibu na kutokomeza rushwa katika sekta ya umma na binafsi
  • Kukuza, kuwezesha na kuratibu ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama ili kuwa na ufanisi wa hatua na vitendo  katika  kuzuia, kuchunguza, kuaadhibu na kutokomeza rushwa katika sekta ya umma na binafsi
  • Kuimarisha na kulinganisha sera na sheria za ndani za  nchi wanachama zinazohusiana na kuzuiai, kubaini, kuadhibu na kutokomeza rushwa katika sekita ya umma na binafsi

The Southern African Forum Against Corruption (SAFAC)

SAFAC ni mtandao wa taasisi za kupambana na rushwa katika nchi wanachama wa SADC. SAFAC ilianzishwa kufuatia uamuzi wa watunga sera wa SADC walioazimia kuundwe mtandandao wa taasisi za kupambana na rushwa katika kanda hii ili uwe chombo cha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa, makosa ya uhujumu uchumi na makosa mengine yenye kufanana nayo. Taasisi hii ilianzishwa mwaka 2000 Gaborone, Botswana na kuzinduliwa rasmi Julai 2001 Maseru Lesotho.

Lengo kuu la SAFAC ni kuwezesha ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya rushwa na kutoa fursa kukutana na kubadilishana uzoefu na namna nzuri ya kufanya kazi baina ya taasisi za kupambana na rushwa katika ukanda wa SADC. Ibara ya 5 ya Katiba ya SAFAC inafafanua malengo ya SAFAC kwa nchi wanachama.

Lengo la SAFAC  ni kuzijengea uwezo taasisi za kupambana na rushwa katika ukanda wa nchi za SADC ili taasisi hizo ziwe na mikakati mizuri ya kupambana na rushwa sambamba na kuwa na ushirikiano mzuri na wadau wengine wa mapambano dhidi ya rushwa.

SAFAC ina wanchama wapatao 14 toka nchi za Jamhuri ya Angola, Botswana, Jamhuri ya Watu wa Kongo, Ufalme wa  Lesotho, Jamhuri ya Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Africa Kusini, Ufalme wa Swaziland, Jamhuri ya Zambia na  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.