JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

P.O.BOX 377

Mara

Simu: (028) 2620240

Fax (028) 2620012

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Tovuti: www.pccb.go.tz

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mara imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime Ofisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzanai (TRA), Ezekiel Gisante, kujibu shtaka la kupokea hongo ya TSh.15,000,000/= toka kwa mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi aliyekuwa akisafirisha vifaa vyake kutoka Kenya kuja Tanzania kupitia mpaka wa Sirari,Tarime.
Mshtakiwa alifikishwa mahakamani tarehe 17/11/2016 mbele ya hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, mheshimiwa Martha Mpanze, katika shtaka la jinai Namba CC 941/2016. Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Mwinyi Yahya, ulidai mbele ya mahakama kuwa mshtakiwa alipokea hongo hiyo toka kwa mfanyabiashara huyo tarehe 13Oktoba, 2016 Tarime, ili aandae taarifa ya uongo ya uhakiki wa ukaguzi wa mzigo wa mfanyabiashara na ilitumiwa na mkuu wake wa kazi kuuruhusu kuingizwa nchini. Aidha upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 15(a)(1) na (2) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Mshtakiwa alikana shtaka.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa uchunguzi wa shauri umekamilika na uko tayari kwa usikilizwaji wa hoja za awali katika tarehe ambayo ingepangwa na mahakama. Mheshimiwa Martha Mpanze alikubali ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hadi tarehe 7Desemba, 2016 itakapotajwa tena. Mshtakiwa alipewa dhamana na mahakama baada ya kutimiza masharti ya dhamana.