JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

MKURUGENZI MTENDAJI – KAS ATEMBELEA TAKUKURU

Leo Septemba 24, 2021 Bw. Tilmann Feltes, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS), alifika TAKUKURU Makao Makuu, Dodoma kwa lengo la kujitambulisha na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. KAS na TAKUKURU, walisaini Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati yao, mwaka 2019 yanayohusu kazi za uzuaji rushwa.

Katika ziara yake, Bw. Feltes aliongozana na ujumbe wa watu akiwemo Bw. Damas Nderumaki ambaye ni Meneja wa Mradi wa ushirikiano huo.